Alizeti hulimwa kwa wingi katika mikoa ya Shinyanga, Singida, Dodoma, Iringa, Tabora, Morogoro, Ruvuma, Mbeya, Arusha, Manyara, na Rukwa. Zao hili hulimwa kwa ajili ya chakula na biashara. MAMBO MUHIMU YA KUZINGATIA WAKATI WA UZALISHAJI Kuchagua aina bora ya mbegu - Chagua aina bora ya mbegu inayovumilia magonjwa, wadudu, inayotoa mazao mengi na kiwango kikubwa cha mafuta. - Vilevile chagua aina ya mbegu ambayo hukomaa kwa wakati mmoja ili kurahisisha uvunaji. KUWEKA MBOLEA - Rutubisha udongo kwa kutumia mbolea za mboji na samadi ili kupata mazao mengi na bora. KUDHIBITI WADUDU NA MAGONJWA Alizeti hushambuliwa na magonjwa ya majani, mizizi na masuke ambayo husababisha upungufu wa mavuno. Hivyo ni muhimu kuyadhibiti ili kupata mavuno mengi na bora. Pia ndege hupunguza mavuno kwa kiasi cha asilimia 50 au zaidi. Njia ya kudhibiti ndege ni kwa kuwafukuza na kupanda mbegu zinazokomaa mapema. MAANDALIZI KABLA YA KUVUNA; UKAGUZI Kagua shamba kuona kama alizet...