Mpango wa Marekani kupeleka watu Mars kufikia 2030

MchoroHaki miliki ya pichaSCIENCE PHOTO LIBRARY
Image captionMchoro: Binadamu wa kwanza atatia guu Mars lini?
Rais wa Marekani Barack Obama amesema serikali ya taifa hilo itashirikiana na kampuni za kibinafsi katika mpango ambao unatarajiwa kuwezesha binadamu kwenda Mars kufikia miaka ya 2030.
Rais Obama alitangaza mpango wake wa kupeleka binadamu Mars mwaka 2010.
Lakini mpango wa idara ya anga za juu ya Marekani Nasa wa kutimiza ndoto hiyo umekosolewa vikali, hasa na Bunge.
Kwenye makala aliyoandika, Rais Obama ameahidi kufanya kazi kwa pamoja na kampun za kibinafsi "kuunda mazingira mapya ambayo yanaweza kuhifadhi na kusafirisha wana anga".
"Tumeweka lengo lililo wazi kwenda katika sura nyingine ya historia ya Marekani katika anga za juu: nayo ni ya kutuma binadamu Mars miaka ya 2030 na kuwarejesha salama duniani. Katika hili kuna ndoto kuu kwamba wakati mmoja binadamu wataweza kwenda huko na kukaa kwa muda mrefu kiasi," Obama alisema kwenye makala katika tovuti ya kituo cha runinga cha CNN.Matamshi yake si ya kushangaza: Nasa tayari wanafanya kazi kwa karibu na sekta ya kibinafsi kupeleka vifaa, mitambo na mahitaji mengine Kituo cha Anga za Juu cha Kimataifa (ISS).
Mars shipHaki miliki ya pichaSPACEX
Image captionBw Musk anataka binadamu wa kwanza waende Mars mwaka 2022
Kampuni nyingi za kibinafsi, sana SpaceX, ambayo chombo chake cha Dragon hutumiwa kupeleka mizigo ISS, zimeweka wazi ndoto ya kupeleleza Mars.
Mwezi uliopita, Elon Musk, mwanzilishi wa SpaceX, alitangaza mpango wake wa kupeleka binadamu wakaishi Mars.
Baadhi walikosoa mpango huo wake wakisema ni ndoto isiyo na uhalisia wowote, lakini wengine wamemsifu kwa kutoa mpango wenye maelezo ya kina wenye lengo la kupeleka binadamu Mars.

Comments

Popular posts from this blog

Viumbe wenye vichwa viwili

Kiboko – Mnyama Mwenye Mdomo Mkubwa Kuliko Wote Duniani

Vituko 10 vya Simu za Kichina