Mpango wa kupeleka watu wakaishi Mars
Haki miliki ya picha AP Image caption Bw Elon Musk Mjasiriamali Elon Musk ametangaza mpango wake wa kuunda makao ya binadamu katika sayari ya Mirihi (Mars kwa Kiingereza),ingawa wanaotaka kunufaika watahitajika kulipa pesa nyingi. Tiketi ya kusafiri hadi kwenye sayari hiyo inakadiriwa kugharimu takriban $200,000. Bw Musk, aliyeanzisha kampuni ya kibinafsi ya usafiri wa anga za juu kwa jina SpaceX, alitangaza mpango huo katika kongamano la kimataifa la wataalamu wa anga za juu (IAC) mjini Guadalajara, Mexico, Jumanne. Mpango wake, unajumuisha mfumo wa usafiri ambao utaweza kusafirisha watu 100 hadi Mars, safari yote ikichukua siku 80. Baadaye, safari hiyo inatarajiwa kuchukua siku 30 pekee. Bw Musk amesema ili kufanikiwa na kuhakikisha gharama kwa kila mtu ni $200,000, basi lazima kuwe na njia ya kutumia tena mitambo ya uchukuzi itakayotumiwa. Haki miliki ya picha SPACEX Image caption Bw Musk anataka binadamu wa kwanza waende Mars mwaka 2022 Amezungumzia mpango wa kuunda kolo...